Thursday, July 26, 2012

MBUNGE ZITTO KABWE

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), alisema Kampuni ya mtandao ya Onmobile inashirikiana na makamupni ya simu za mikononi kuwanyonya wasanii kwa kuwalipa asilimia ndogo ya mapato yanayotokana na matumizi ya nyimbo zao. Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliyosomwa bungeni mjini Dodoma jana, Zitto alisema kinachoshangaza kampuni hiyo iliyohodhi mambo yote ya kampuni za Vodacom na Airtel, inafanya kazi bila leseni. “Ukimpigia simu Waziri Mkuu… utasikia simu yake ina wimbo wa Rose Mhando, Naibu Waziri Adam Malima yeye upo wimbo wa Dar mpaka Moro wa Wanaume Familly na ukinipigia mimi utasikia Kurani ama wimbo wa CHADEMA. “Lakini kinachoshangaza wasanii hawa wananyonywa licha ya nyimbo zao kutumika, tunadhani wasanii wanapata… si kweli kwani hata vituo vya redio na televisheni vya serikali vinatumia nyimbo hizi bila kuwalipa chochote. Makampuni makubwa ya Vodacom na Airtel wameingia mkataba na Onmobile na wanaingiza sh bilioni 43 kutokana na milio,”

No comments:

Post a Comment